Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry amewaambia mashabiki wa Arsenal kuwa kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger hatakiwi kuondoka klabuni hapo, lakini amekiri kuwa kocha huyo ana kazi ya ziada kuibadili klabu hiyo kuwa na kariba ya kugombea ligi kuu ya Uingereza.
Imekuwa miaka 13 tangu mzee Wenger atwae taji la ligi kuu ya Uingereza alilolitwaa mara tatu tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 1996. Henry aliyejiunga na Arsenal chini ya Arsene Wenger amekiri kuwa kazi ni kubwa mbele lakini Wenger sio wa kuondoka.
"Binafsi, nadhani Arsene hatakiwi kuondoka," Henry, ambaye alipewa nafasi ya kikosi cha kwanza na Wenger katika klabu ya Monaco akiwa na umri wa 17, aliiambia RMC. "Kuhusu kubadili mbinu na aina ya uchezaji? Sina uhakika kama yupo tayari. Lakini kazi anayotakiwa kufanya sasa hivi inahusisha mambo mengi kama suala la kiakili.
"Mbinu zinasaidia, lakini kile nilichokiona [walipopoteza 3-1 dhidi ya Chelsea], it's lilikuwa tatizo la kiakili/kifikra. Ni kitu nilichokiona kwa muda mrefu kiasi sasa. Na hapo ndipo ugumu wa kazi wa Wenger ilipo na inapoendelea kuwa ngumu zaidi, kwa sababu ni tatizo lililo kifikra zaidi. Sio rahisi kulitatua.
"Arsenal hawajashinda ubingwa kwa miaka 12, na unaweza kuamini kuwa hawawezi kushinda kwa msimu huu. Nahisi kuna ubora kwenye kikosi chao. Inajitosheleza kushinda ubingwa? Mwanzo wa msimu, ulikuwa ukitizama Chelsea na Arsenal kwenye karatasi, hapakuwa na tofauti kubwa, hivyo inawezekana.
Comments
Post a Comment