Heineken waendelea kunogesha UEFA Champions League.


Heineken waendelea kunogesha UEFA Champions League.

Kwa sisi wapenzi wa michuano ya UEFA Champions League mara zote huwa tunafurahia kuona matangazo ya kibunifu ya Heineken muda wa mapumziko, mwanzo na mwisho wa mechi.

Wale washkaji zangu wanafurahia mechi wakiwa na bucket zao za Heineken najua mnazikumbuka zile chupa za limited edition za UEFA Champions. Basi sasa hivi uhusiano wa UEFA na Heineken umenogeshwa zaidi.

Leo tarehe 12/2/2017 Heineken imetangaza kuongeza makubaliano ya kuendelea kuwa wadhamini wa michuano maarufu ya vilabu duniani UEFA Champions League kwa misimu mitatu ijayo hadi mwaka 2021. Makubaliano haya mapya yanahusisha na UEFA Super Cup kwa mwaka 2018,2019 na 2020. Uhusiano huu mpya unandelea na kuongezea ukuaji na mambo mbalimbali yanayohusu Heineken duniani.

Global Sponsorship director wa Heineken Hans Erik Tuijt kuhusu hili amesema,"Heineken imefurahia uhusiano huu na UEFA kwa zaidi ya miaka 20. Pia tunatumaini utaendelea kunufaisha kwa miaka inayokuja. UEFA Champions League ni sehemu nzuri ya kuihusisha Heineken na vitu vyake duniani kote kuanzia Sao Paolo hadi Shanghai. Kampeni yetu ya dunia nzima 'Champion the Match' imeweza kuhusishwa kwenye masoko zaidi ya 100 duniani. Pamoja na tour ya kombe la UEFA imeleta experience nzuri zaidi ya dakika 90 za mechi. Uhusiano huu unaleta matokeo chanya kwenye sehemu nyingine ambazo tupo kama Formula One, Rugby, World Cup na James Bond."

General Manager wa Heineken East Africa Uche Unigwe alivyokua anaongea na wafanyakazi kwenye ofisi za Nairobi alisema, "Tuna furaha ya kuwa wadhamini wa UEFA kwa miaka 3 mingine ambayo inaonyesha jinsi tulivyona nia na madhumuni ya ku-support mchezo huu. Tuna furaha zaidi kwa kuongeza uhusiano wa Heineken Brand na UEFA Champions na mashabiki wake wenye shauku kubwa ndani ya Afrika Mashariki".

Unahitaji kujua kwamba Heineken imekua pamoja na UEFA Champions League tangu mwaka 1994. UEFA Champions League imekuwa inaangaliwa na watu 4.3 billion duniani. Pia Heineken imewezesha kuafanyika tour ya kombe la UEFA tangu mwaka 2007 na kufika kwenye nchi 35 narani Asia,  Africa, North and South America.

Mechi za UEFA zitaendelea wiki hii siku ya Jumanne kama zinavyoonekana hapo chini.

 



Comments