NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', amerusha kombora Simba baada ya kusema watahakikisha wanaifunga timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ili waweze kuwa katika mazingira bora ya kutetea ubingwa wao.
Akizungumza jana, Cannavaro alisema mchezo huo utakaochezwa Februari 25 mwaka huu, utaamua hatima ya wao kutetea taji lao.
Cannavaro alisema wamejipanga kuondoka na pointi tatu ambazo zitawaweka katika mazingira bora zaidi ya kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo na baadaye kutetea ubingwa wao.
"Simba acha wachonge, lakini dawa yao ni sana," alisema Cannavaro.
Alisema wanapiga kelele huku wakijua wazi hawana uwezo wa kuifunga Yanga.
"Sisi tunawaheshimu Simba kama zilivyo timu nyingine katika ligi, lakini pia hatuwaogopi kwa kuwa tunajua dawa yao iko wapi hawawezi kupata ubingwa kupitia sisi," alisema.
Comments
Post a Comment