Cameroon imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) baada ya kuwafunga Ghana mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili uliofanyika usiku huu mjini Frenceville nchini Gabon.
Michael Ngadeu-Ngadjui alianza kuipatia Cameroon bao la kuongoza dakika ya 72 ambapo kabla ya sekunde chache refa kupuliza kipenga cha mwisho Christian Bassogog aliipa timu hiyo goli la pili na la ushindi.
Magoli hayo mawili yanawapa Cameroon nafasi ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.
Cameroon itakutana na Misri ambayo ilitinga hatua ya fainali jana baada ya kuwafunga Burkina Faso goli 4-3 kwa mikwaju ya penalti.
Fainali hiyo itachezwa Jumapili ijayo ambapo itatanguliwa na mechi ya kusaka mshimdi wa tatu siku ya Jumamosi kati ya Ghana na Burkina Faso.
Comments
Post a Comment