BENFICA YAKANUSHA KUMPIGA BEI VICTOR LINDERLOF



BENFICA YAKANUSHA KUMPIGA BEI VICTOR LINDERLOF
KLABU ya Benifica ya Ureno imekanusha tetesi za kumuuza mlinzi kijana Victor Linderlof mwenye umri wa miaka 21.

Hatua ya klabu hiyo kukanusha inafuatia taarifa za kwamba timu kubwa za barani Ulaya zimeingia vitani kwa ajili ya kusaka saini yake.

Timu mahasimu katika La Liga, Real Madrid na Barcelona ni kati ya vigogo wanaotaka kumsajili wakati wa kipindi cha usajili cha dirisha la Januari mwakani.

Pamoja na vigogo hao vya Ligi ya Hispania pia Manchester United wanatajwa katika mbio hizo za kumwania nyota huyo wa klabu ya Benfica.

Mlinzi huyo kijana amekuwa katika kiwango bora katika msimu huu kiasi cha kuzigonganisha timu kubwa kupata saini yake.

Imebainika kuwa Benfica imesitisha nia ya kumweka sokoni beki huyo baada ya kuondokewa na mlinzi wao mahiri Renato Sanches aliyejiungana Bayern.


Katika kuhakikisha Haimpotezi Lindelof, imeamua kuweka mezani ofa kubwa ya euro mil 40 ambapo imebainika klabu ya Barca na Madrid wanaweza wasipande dau hilo.


Comments