KIGOGO wa Bundesliga na mabingwa watetezi wa Ujerumani, Bayern Munich wamesema hawana haja ya kufanya usajili wa kutisha kutokana na ukweli kuwa kikosi chao kipo kamili na kimetimia.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo kongwe alithibitisha taarifa za kutosajili katika usajili wa majira ya kiangazi.
"Hatuna tulichokipanga kuhusu usajili mpaka sasa. Ni sawa na kusema, hatuna haja ya kufanya hivyo labda itokee lolote la dharura," alisema Sammer.
"Tuna wachezaji wachache wa kuwarejesha kikosini Holger Badstuber amerudi na David Alaba pia amerudi katika kiwango chake."
"Tumemuuliza kocha wetu kuhusiana na suala la kusajili akatuhakikishia kuwa hakuna haja ya kufanya usajili mkubwa akiamini kuwa kikosi kipo imara kwa ajili ya msimu huu."
"Ila tumempa fursa ya kuangalia kama anaweza kufanya usajili katika muda mwafaka, nae amejibu kuwa ataangalia kama kuna haja ya kuongeza wawili ama watatu, ila amejiridhisha kuwa na kikosi bora cha kutetea ubingwa kwa mara nyingine msimu huu," alisema Mkurugenzi huyo.
Comments
Post a Comment