Miamba wa soka wa Hispania Fc Barcelona wameanza vibaya hatua ya kumi na sita bora baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 ugenini dhidi ya Psg ya Ufaransa.
Angel di Maria alianza kuwaandika Pgs goli kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja nyavuni, katika dakika ya 40 mshambuliaji mpya wa Wafaransa hao Julian Draxler akaongeza bao la pili.
Dakika ya 55 Angel di Maria tena akawachapa Barca bao la tatu, kabla ya Edinson Cavan kuhitmisha shughuli kwa bao la nne .
Katika mchezo mwingine Benfica ya Ureno wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Borrrusia Dotmund ya Ujeruman kwa bao la Konstantinos Mitroglo.
Ligi hiyo itaendlea tena leo kwa michezo miwili Bayern Munich wakiwalika Arsenal nao Real Madrid wakiwa wenyeji wa Napoli.
Comments
Post a Comment