KUNA kauli ambayo kocha wa Chelsea alimwambia Cesc Fabregas inayoonyesha kumshusha presha kiungo huyo.
Unajua amemwambiaje? Antonio Conte amemwambia kiungo huyo raia wa Hispania kuwa asikate tamaa ya kubakia Stanford Bridge kwani amemweka katika orodha ya wachezaji muhimu kikosini.
Lakini Conte amemweleza fabregas kuwa pamoja na kauli hiyo, lazima akaze buti kwani ushindani ni mkubwa ndani ya msimu huu.
Kauli ya kocha wa matajiri hiyo inakuja siku chache ambapo kiungo huyo amekuwa akipangwa katika mechi nyingi muhimu.
"Cesc yumo katika mipango yangu ya kuimarisha kikosi cha msimu huu."
"Ninachoshukuru ni kwamba ni mmoja ya wachezaji walio na uzoefu mkubwa wa Ligi, msaada mkubwa."
"Ninampa nafasi katika mechi kadhaa za kuibeba timu na ninaamini ana uwezo wa kuonyesha kiwango chake cha misimu miwili iliyopita," alisisitiza Conte.
Comments
Post a Comment