Almanusura Bill Gates Ainunue Liverpool.


Almanusura Bill Gates Ainunue Liverpool.

Wakati klabu ya Liverpool ikiwa katika fomu mbovu kutokana na kutokupata ushindi katika mwezi januari kwenye ligi kuu ya Uingereza, Taarifa zinasema klabu hiyo ilikuwa inunuliwe na tajiri namba moja duniani na mmiliki wa Microsoft Bill Gates pamoja na mmiliki wa mabingwa wa kihistoria wa Super Bowl, New England Patriots bwana Robert Kraft kipindi ambacho waliokuwa wamiliki wa klabu hiyo Tom Hicks na George Gillett walipoamua kuiuza.
Taarifa zimetolewa na nyaraka zilizopatikana katika mahakama kutokana na taarifa za ushindani wa kisheria kati ya kampuni inayofahamika kama Mill Financial and Gillett na ile ya Royal Bank of Scotland. Hicks na Gillett walikubali kuiuza Liverpool mwezi April 2010 baada ya kushindwa marejesho ya fedha walizokopa wakati wanainunua klabu hiyo mwaka 2007.
Barclays Capital walipewa kazi ya kutafuta wanunuzi, na nyaraka kutoka kwenye kanda ya kiuchumi katika mahakama kuu ya New York County Supreme Court zinaonyesha kuwa Bill Gates, mwanzilishi wa Microsoft, alifuatwa katika yangazo la wahitaji wa kuinunua klabu hiyo.
Martin Broughton, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Liverpool kipindi hicho, aliulizwa kama kulikuwa na ukweli juu ya kufuatwa kwa Bill Gates na Bob Kraft, akajibu "ni kweli kabisa"
Broughton aliulizwa pia kama alikuwa anafahamu kama Barclays Capital walikuwa wanafuatilia jitihada zilizokuwa zinafanywa na wawekezaji wa Hong Kong, Norway.
Alijibu kwa kusema, utafutaji wa wawekezaji wapya ulifanyika katika kila bara na ulihusu kuwasiliana na watu tofauti duniani kote.  Bill Gates hakujibu au kuitikia wito lakini Kraft alisita katika kuinunua klabu hiyo huku pia akiwa alikataa ofa ya David Moores mwaka 2005.
New England Sports Ventures, wanaofahamika kama Fenway Sports Group, hatimae waliinunua Liverpool kwa dau la £300 million mwezi October 2010, huku Hicks na Gillett wakisema dili lile lilikuwa wizi wa mchana.



Comments