Taarifa Kuhusu Mchezaji Emmanuel Adebayor Kuja Kucheza Yanga ya Tanzania Hii Hapa




Taarifa Kuhusu Mchezaji Emmanuel Adebayor Kuja Kucheza Yanga ya Tanzania Hii Hapa
Emmanuel Adebayor 
Jana January 25 2017 moja kati ya taarifa zilizokuwa zimeenea katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Togo aliyewahi kucheza Arsenal, Man City, Tottenham Hotspurs na Crystal Palace  Emmanuel Adebayor kuripotiwa kujiunga na  timu ya Yanga.

Habari kutoka soka25east.com na mitandao mingine mitatu ya Kenya zilisema kuwa staa huyo atajiunga na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga ambayo pia inachezewa na Vincent Bossou anayechezea timu moja ya taifa na Adebayor na walikuwa pamoja AFCON juzi.

Saa 24 baada ya taarifa hizo kupita mitandao ya Skysports na BBC SPORTS imeripoti na kumnukuu Adebayor kuhusu mpango wake wa sasa katika soka akiwa mchezaji huru, anasema bado ana mpango wa kurejea ligi kuu England na hajaizungumzia Yanga hata tone, hiyo imedhihirisha kuwa tetesi za kujiunga na Yanga sio za kweli.

"Nimepokea ofa chache kutoka timu za ligi kuu England na wote mnajua napenda kucheza England, licha ya kuwa mimi sio moja kati ya wachezaji wanaopendwa England nimecheza England kwa miaka kumi, ieleweke pia sikuja AFCON kucheza ili nipate timu nilikuja kuwakilisha taifa langu"


Comments