POBGA AIPELEKA MANCHESTER UNITED FAINALI YA EFL CUP ....Hull yatibua yahitimisha safari ya 'unbeaten' kwa ushindi wa 2-1


POBGA AIPELEKA MANCHESTER UNITED FAINALI YA EFL CUP ....Hull yatibua yahitimisha safari ya 'unbeaten' kwa ushindi wa 2-1

Hull City imehitimisha safari ya Manchester United ya kutokufungwa (unbeaten) baada ya kushinda 2-1 katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya EFL Cup.

Hata hivyo ni Manchester United iliyofanikiwa kutinga fainali kufuatia ushindi wao wa 2-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Old Trafford.

United sasa itaumana na Southampton katika fainali itakayochezwa Wembley Februari 26.

Tom Huddlestone aliifungia Hull bao la kwanza kwa penalti tata kunako dakika 35, lakini bao la kusawazisha la Paul Pobga la dakika ya 66 lilitosha kuwapeleka United fainali licha ya bao la pili la wenyeji lililokwamishwa wavuni na Oumar Niasse dakika tano kabla ya mpira kumalizika.

Ushindi huu ni wa kwanza kwa Hull City dhidi ya Manchester United tangu mwaka 1974 na umehitimisha safari ya mechi 17 bila kufungwa ya vijana hao wa Jose Mourinho. 

Hull (4-4-2): Marshall 6.5; Meyler 6, Maguire 6.5, Dawson 7.5, Tymon 6; Maloney 6 (Evandro 64 6.5), Huddlestone 7, Clucas 6.5, Diomande 6 (Hernandez 70 6); Bowen 6.5 (Markovic 59 6), Niasse 6.5

Man Utd (4-2-3-1): De Gea 6; Darmian 6, Jones 6, Smalling 6.5, Rojo 5.5; Herrera 6, Carrick 5.5; Lingard 6 (Rooney 79 6), Pogba 6.5, Rashford 7 (Fellaini 90); Ibrahimovic 6





Comments