"NI CHELSEA TU NDIO IMEBAKI KWENYE MBIO ZA UBINGWA" WENGER ADAI



"NI CHELSEA TU NDIO IMEBAKI KWENYE MBIO ZA UBINGWA" WENGER ADAI
BAADA ya Chelsea kushinda mechi 12 mfululizo kabla ya mechi ya Jumamosi, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger fasta amedai: "Timu moja tu Chelsea ndio imebaki kwenye mbio za ubingwa."

Wenger haoni uwezekano wowote wa Liverpool, Man City, Man United, Tottenham wala timu yake kutwaa taji msimu huu isipokuwa timu hiyo ya darajani.

Hata hivyo, bosi wa Chelsea, Antonio Conte anakosoa utabiri wa Wenger na kudai kwamba Ligi ndio kwanza mbichi na ubingwa hauko mikononi mwao.

"Nadhani ni vigumu sana kujibu swali hili. Tumecheza mechi 18 bado kuna mechi nyingine 20 kumalizia msimu huu."

Mwanzoni mwa msimu huusio kocha, mwandishi wa habari wala mtu yeyote aliyetegemea Chelsea ingekuwa miongoni mwa timu zinazotajwa kutwaa ubingwa na hiyo ni kutokana na msimu mbaya uliotangulia.

"Hatukufanya vizuri kwenye soko la wachezaji lakini sasa nimefurahi kuona mambo yamebadilika. Nina shaka kidogo ninapopata mabadiliko mazuri haraka haraka kiasi hiki. Hii inanifanya niwe makini."

"Tuko mbele kwa pointi sita tu dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili na pointi saba timu katika nafasi ya tatu."
"Nadhani safari ni ndefu, nimefurahishwa na jinsi wachezaji wangu wanavyopitia mabadiliko mazuri."


"Jambo la muhimu kwetu ni kuhakikisha tunapigana kwa nguvu zaidi, akili yetu iwe kwenye soka kushinda mechi 12 hazitoshi kusema sisi tayari mabingwa msimu huu."


Comments