MARCO Reus bado anaonekana mtamu kwa klabu mbalimbali Ulaya hii ni kutokana na kuwepo kwa taarifa za kiusajili kuwa vigogo wa England navyo vimeingia vitani kwa ajili ya usajili wa kiangazi mwaka huu.
Man United Chelsea na Tottenham Hot Spurs wamo katika vita ya kupigana vikumbo kumwania.
Nyota huyo raia wa Ujerumani alizikosa fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Brazil kutokana na kuwa majeruhi na sasa yupo katika kiwango kizuri ndani ya Borrusia.
Lakini vigogo Man City, United na Arsenal wametajwa katka vita ya kumwania straika huyo ambaye anawindwa pia na vinara wa Bundelisliga na Bayern.
Daily Star Limelipoti pia taarifa za Real Madrid kuingia vitani kwa ajili ya Reus lakini wameeleza pia ugumu kwa mshambuliaji kinda wa Liverpool Rahhem Sterling.
Mwanandinga mwingine anayezitoa udenda klabu kubwa Ulaya ni pamoja na Pierre Aubabiyang pia wa Borrusia Dortmun.
Comments
Post a Comment