"KUNA KITU CHA KUONGEZA HAPA ARSENAL" ASEMA KOCHA ARSENE WENGER



"KUNA KITU CHA KUONGEZA HAPA ARSENAL" ASEMA KOCHA ARSENE WENGER
KOCHA Arsene Wenger ni kama kabaini upungufu katika kikosi chake cha Arsenal baada ya kusema kuwa kinahitaji kitu maalum cha kuongeza baada ya Olivier Gioroud kufunga bao dakika za mwisho lililofanya iondoke na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya West Brom.

Katika mchezo huo wa majuzi uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates, Gunners walikizidi nguvu kikosi cha Tony Pulis lakini ukuta wa Baggies ukawa imara.

Hata hivyo Arsenal ambao walikuwa wameshapoteza mechi mbili za Ligi Kuu kwa kufungwa mabao 2-1, baadae walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Giroud zikiwa zimebaki dakika nne baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na Mesut Ozil.

"Mwisho wa yote tulitakiwa kuwa wavumilivu kutokana na kuwa tulikuwa tukicheza na kikosi cha West Brom ambacho kilikuwa kimejipanga," Wenger aliwaambia waandishi wa habari.

"Walikuwa wamejipanga vizuri ili wasifanye makosa katika safu ya ulinzi na kama walivyofanya isingekuwa rahisi kuwafunga," aliongeza kocha huyo.


Alisema kuwa walipata nafasi nyingi na kupiga mashuti mengi lakini bado kuna kitu maalum.


Comments