Mtanzania Mbwana Samatta anayeichezea timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, usiku wa January 21 2017 alirudi tena kwenye headlines baada ya kuisaidia timu yake ya KRC Genk, kutoka na point tatu ugenini katika uwanja wa Stadion am Kehrweg dhidi ya wenyeji wao AS Eupen.
Mbwana Samatta ambaye alipata nafasi ya kucheza kwa dakika zote 90, alifanikiwa kuipatia ushindi wa goli 1-0 timu yake ya KRC Genk dhidi ya AS Eupen dakika ya 82 ya mchezo, baada ya kupiga kichwa mpira wa kona uliyopigwa na Ruslan Malinovskiy.
Katika mchezo huo KRC Genk ambao wapo nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji inayoshikisha timu 16, licha ya kuwa ugenini waliutawala mchezo kwa asilimia 55 na wenyeji wao ambao wapo nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji, walimiliki mpira kwa asilimia 45.
Comments
Post a Comment