Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema klabu yake inatafakari uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa nahodha John Terry wakati wa mechi ya kombe la FA Jumapili.
Katika mechi hiyo Chelsea wali ifunga Peterborough 4-1.
Chelsea walikuwa mbele 3-0, Terry, 36, alimwangusha mshambuliaji Lee Angol na refa Kevin Friend akaamua kuwa alikuwa mchezaji wa mwisho wa Chelsea.
"Lazima uheshimu uamuzi, lakini wakati huu labda tutakata rufaa," alisema Conte.
Ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Terry kuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi tangu Oktoba.
Chelsea wakishindwa kwenye rufaa hiyo, basi Terry hatakubaliwa kucheza mechi ya Ligi ya Premia ugenini kwa mabingwa watetezi Leicester City tarehe 14 Januari.
John Terry ameoneshwa kadi tatu kati ya sita nyekundu walizoonyeshwa wachezaji wa Chelsea hivi karibuni.
Comments
Post a Comment