Wilfried Bony amtaja Wakala Tapeli.. Amfikisha Kizimbani


Wilfried Bony amtaja Wakala Tapeli.. Amfikisha Kizimbani

bon

Mchezaji wa klabu ya Manchester City ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Stoke City, Wilfried Bony amejipanga kumfungulia mashitaka wakala wake wa zamani pamoja na klabu ya Swansea City katika jitihada za kurejesha kiasi cha paundi milioni 8 ambayo anaamini ni mapato yake aliyoingizwa mjini na kuyapoteza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, akikipiga kwa mkopo katika klabu ya Stoke City, amemfungulia mashitaka wakala wake wa zamani ambaye pia alikuwa mwakilishi wake, Francis Kacou kuhusiana na fedha zilizochukuliwa pasipo ruhusa yake katika usajili ulimhusu yeye akitokea klabu ya Vitesse Arnhem kwenda Swansea mwaka 2013 na baadae alipoelekea katika klabu ya Manchester City mwaka 2015. Bony pia anaishutumu klabu ya Swansea kuwa ilikuwa inafahamu mchezo mzima.

Malalamiko ya awali yalifunguliwa katika jiji la Manchester siku ya Jumanne wiki hii lakini kusikilizwa kwa mashitaka hayo kumehairishwa kutokana na kusubiriwa kwa maamuzi ya wapi kesi hiyo inatakiwa kusikilizwa. Kacou, pamoja na mfanyabiashara mwenzie Dalibor Lacina, pia wameomba muda ili waweze kukusanya taarifa sahihi na ushahidi kwa utetezi wao.

Wilfried Bony is taking action against Swansea City and            his former agent to recover £8m

Lakini kama inavyoweza kuwa bahati mbaya, Kacou atakuwa anagombea nafasi katika mkutano mkuu wa Nchi ya f Ivory Coast National Assembly siku ya Jumapili, December 18 ambayo kama atashinda inaweza kumpa kinga ya kisiasa kwa maana ya kukwepa kesi yake kusikilizwa nchini Uingereza.

Kacou pia amekuwa katika mgogoro na winga na mchezaji wa Bournemouth Max Gradel na beki wa zamani wa vilabu vya Arsenal na Sunderland, Emmanuel Eboue ambaye anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kujihusisha na soka kutokana na kushindwa kumlipa wakala wake.

Swansea walilipa kiasi cha paundi milioni 12 (£12million) kwa  Vitesse kumsajili Bony na baadae akajiunga na Manchester City kwa kiwango kinachokadiriwa kuzidi paundi milioni 25 (£25m).

Kacou has also been in dispute with Bournemouth forward            and Bony's compatriot Max Gradel

Bony yupo katika mkopo katika klabu ya Stoke City yenye maskani yake kwenye uwanja wa Britannia lakini ana kipengele kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuuzwa kwa klabu ya China mwezi Januari kama atahitajika.

Msemaji wa Swansea City alisema: 'Hili ni jambo linalomhusu Bony pamoja na wawakilishi wake, sie hatumo.'

'Bahati mbaya tumeingizwa kwenye matatizo yake kwa sababu tu tulihusika katika kuuzwa kwake mara zote mbili, mara ya kwanza ikiwa kumleta hapa na nyingine ikiwa kumuuza kwenda Manchester City.'



Comments