Manager wa Arsenal ambao na wao bado wapo kwenye mbio za kukimbiza ubingwa na kuacha tabia yao ya kuishia nafasi ya nne kila msimu, ameipa shavu Chelsea kushinda ubingwa wa ligi msimu huu.
Wenger alikua kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema kwa sasa anaipa nafasi kubwa Chelsea kushindwa ubingwa kwa mwenendo wao,"Kwa sasa Chelsea wana nafasi kubwa kwasababu wametengeneza utofauti mkubwa sana"
Wenger aliendelea,"Lakini bado wanaweza kupoteza kama tunavyojua hapa England. Kwasasa wanaonekana kwamba wanaenda kushinda lakini wanaweza kupoteza hapo baadae. Wamejua matatizo yao vizuri na utampa sifa Conte kwa kutatua hayo matatizo".
Kesho Dec 31 Chelsea watakutana na Stoke City na kujaribu kuendelea kuvuna points muhimu ili wajiweke kwenye nafasi nzuri. Mechi kubwa kwa kesho ni kati ya Liverpool Vs Manchester City
Comments
Post a Comment