Wawa kafanya kweli kwa mzazi mwenzake


Wawa kafanya kweli kwa mzazi mwenzake

BEKI wa zamani wa Azam FC, Serge Pascal Wawa amefunga ndoa na mzazi mwenzake aliyezaa nae watoto watatu.

Wawa amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram picha zinazomuonyesha akiwa na mwanamke huyo katika nyuso za furaha huku akipokea salamu za pongezi toka kwa marafiki  kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Wawa amerejea kwenye timu yake ya zamani ya El-Merreikh ya Sudan baada ya kumaliza mkataba wake na matajiri wa Ligi Kuu ya Vodacom na hakutaka kuongeza mkataba kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokuwa na uhusiano mzuri na Kocha Mhispania, Zeben Hernandez.wawa-ndoa

Chanzo: boiplus.blogspot.com



Comments