Wachezaji wawili wa ambao inabidi wajiunge na Mbeya City wanakumbwa na utata mkubwa kutoka kwa bosi wao wa zamani "Zamunda".
Tatizo la wachezaji hawa tayari lipo mahakamani na wakili wa wachezaji hawa bwana Charles Tumaini ametoa ufafanuzi kuhusu tatizo hilo,"Mbeya City wanawataka hawa wachezaji, hawa wachezaji walikua wanacheza African Lyon kwa half season only kwa mkataba wa kukubaliana tu. Hawakua na mkataba ambao umeandikwa rasmi. Kitu cha kushangaza kabisa hawa wachezaji walitakiwa kuwa na mkataba wao kama professional na copy zingekua kwao, African Lyon na TFF. Lakini walipokuja kwetu kutupa hii kazi tulivyowauliza walisema hawakuadikishwa mkataba wowote lakini walikua na risiti ambayo walilipwa kama singing fee dola 500 na inaonyesha ni half season."
"Season imeisha na hawana mkataba na African Lyon , Mbeya City anawataka. Boss wao Zamunda anakataa anasema hao ni wachezaji wangu.Lakini kabla ya hapo wakati mgogolo wa pesa ulivyokuwaga aliwapa ticket akawambia nendini ubungo pendeni basi nendeni hadi Kagera muende kwenu. Zile ticket tunazo, na wale wachezaji wakaamua basi tunaachana nae tunatafuta timu nyingine ambayo ni Mbeya City. Sasa hapo ndipo tena Zamunda anakuja na kusema hao ni wachezaji wangu."
"Alitaka waondoke ili kesi yao isiwe na nguvu lakini baada ya kuona kwamba wanapata kazi nyingine ndio anakuja kwamba huyu ni mchezaji wangu. Nimeenda hadi TFF hawa wachezaji hawana mikataba, TFF wakasema hawana mikataba yao na tumemwambia Zamunda alete lakini hazijaja. Tumeangalia passport zao ambazo alikua amezishikiria Zamunda zinaonyesha kamba zipo blank na hawana hata kibali cha kufanya kazi hapa Tanzania. Baada ya kuwafukuza hata zile ticket zenyewe hazikua hazijalipiwa sasa sijui alikua anataka wasafiri vipi"
Shaffih Dauda alihoji kuhusu wachezaji hawa kuwa na ITC ili waweze kuingizwa kwenye system ya wachezaji wa EPL, jibu likawa kwamba wachezaji hawa hawakua hata na ITC kitu ambacho kinaonyesha hawapo kwenye record au kama wapo basi imeongopwa kwamba ni watanzania wakati sio.
Comments
Post a Comment