Timu ya wanawake Nigeri imeandamana kudai posho


Timu ya wanawake Nigeri imeandamana kudai posho

img-20161214-wa0026

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka la wanawake Nigeria 'Super Falcons', wameingia barabarani wakiandamana wakiwa na mabango ili kushinikiza malipo yao baada ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake (Women Afcon).

Wachezaji hao wa timu ya wakubwa, wameandamana hadi Bungeni kwa ajili ya kufikisha ujumbe wao wa kwa rais wa Nigeria  Muhammadu Buhari.

img-20161214-wa0024

Buhari atahudhuria Bungeni leo kusikiliza bajeti ya 2017, wanaandamani hao watasubiri hadi wakati rais atakapofika ili kufikisha ujumbe wao.

Baada ya kushinda taji la Africa Women's Cup 2016 of Nations, wachezaji hao wameendelea kukaa hotelini mjini Abuja wakishinikiza kulipwa stahiki zao na shirikisho la soka la Nigeria (Nigeria Football Federation, 'NFF').

img-20161214-wa0023

Kila mchezaji aliahidiwa kitita cha dola za marekani 16,500 endapo wangeshinda kombe hilo lilifanyikia Cameroon lakini badala yake wamelipwa kiasi kisichozidi dola 1, 900 kwa kila mmoja.

Mbali na madai hayo yanayotokana na ushindi wa kombe la Afrika kwa wanawake, wachezaji pia wanadai posho zilizotokana na mechi zao za kufuzu  AWCON.

img-20161214-wa0025

NFF pamoja na Wizara ya Michezo ya Nigeria wamekuwa wakitoa ahadi kedekede ambazo mwisho wake wameshindwa kuzitekeleza.



Comments