UPO              uwezekano kuwa takwimu zina nafasi kubwa ya kutoa majibu ya              ukweli kuliko kinyume chake.
        Kama              unabisha sikiliza takwimu za mastaa wawili wa (Chelsea)              Diego Costa na (Manchester City) Sergio Aguero.
        Wataalam              hawa wa kutikisa nyavu za lango Ligi Kuu England walikuwa na              mabao 20 kwa jumla yao, huku kila mmoja akigusa nyavu mara              10.
        Lakini              kabla ya mechi ya jana baina ya timu hizo, Costa alikuwa na              mchango mkubwa wa mafanikio kwa timu yake kuliko Aguero wa              Manchester City.
        Costa              alikuwa ametoa pasi nne za mabao na kutengeneza nafasi 22 za              kufunga, wakati Aguero hajatoa pasi yoyote ya bao kwa              wenzake.
        Pia              Costa alikuwa amewania mipira mingi ya kichwa kuliko Aguero.
        
Comments
Post a Comment