Kiungo kinda wa Azam FC, Farid Mussa ameanza maandalizi yake tena kujiandaa kwenda Hispania kujiunga na timu yake ya Derportivo Tenerife ya Hispania.
Tayari Farid amepata matumaini mapya baada ya leo kutinga kwenye ubalozi wa Hispania na kuanza kushughulikia kibali cha kufanya kazi nchini humo.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amethibitisha kwamba mambo yanakwenda vizuri.
"Kuna matumaini makubwa kwamba sasa mambo yataenda vizuri na Farid alikuwa ubalozini kwa kuwa tayari klabu ya Tenerife imeishawasiliana na ubalozi wa Hispania hapa nchini," alisema.
Awali kulikuwa na hofu ya kuua kipaji chake kwa kuwa suala la kibali kilionekana kuwa tatizo huku Farid akiendelea kukaa benchi kwa kuwa hawezi tena kuichezea Azam FC.
Comments
Post a Comment