KIUNGO wa timu ya Paris Saint-Germain, Marco Verratti ni kama kaziponda timu za Barcelona na Real Madrid baada ya kusema kuwa hazina ubavu wa kushinda mabao 5-0 kama zingekuwa zinashiriki kwenye michuano ya igi Kuu Ufaransa "Ligue 1" kama zinavyofanya kwenye La Liga.
Akizungumza juzi Verratti ambaye amekuwa akikipiga kwenye klabu hiyo ya PSG tangu mwaka 2012 alisema kuwa Ligi yao imekuwa haipewi umuhimu wa kutosha kama zilivyo nyingine kubwa Ulaya.
Muitaliano huyo alisema kwamba ushindani na ubora uliopo katika Ligue 1 ni mkubwa na hivyo haoni kama Barca na Madrid kama zingepamba kama zingekuwa zinacheza kwenye Ligi sawa.
"Nchini Ufaransa kuna ushindani mkubwa hata kama timu inashika nafasi ya chini kwenye msimamo na timu hizo ni ngumu unapokutana nazo," Verrati aliandika kwenye ukurasa wa mtandao wa Goal.
"Katika ushindani mwingine mbio zipo tofauti. Kwa mfano nchini Hispania kwa wastani timu kama hizo zinapokutana na eal Madrid ama Barcelona huwa zinasahau ushindani na kucheza soka. Huwa zinatoa mwanya badala ya kulinda," aliongeza nyota huyo.
Alisema kuwa jambo hilo ndilo linafanya Real Madrid ama Barcelona kufunga mabao matano ama zaidi na huku akisisitiza kwamba hana uhakika kama zingeweza kufanya hivyo kama zingekuwa zinacheza nchini Ufaransa.
Comments
Post a Comment