MAOFISA wa Manchester United wameanza              kuchoshwa na tabia za kocha wao Jose Mourinho.
        Mouroinho yuko hatarini kusimamishwa              kukaa kwenye benchi la ufundi baada ya kutolewa uwanjani na              mwamuzi Jon Moss dhidi ya West Ham.
        Alitolewa kufuatia kitendo cha kupiga              chupa teke kupinga nyota wake Paul Pogba kuonyeshwa kadi ya              njano kwenye mechi ya West Ham.
        Maofisa wa Manchester wanalalamika              kichinichini kitendo cha kocha huyo kutuhumiwa makosa ya              chama cha soka cha England (FA) kwa mara ya tatu katika              kipindi cha mwezi mmoja.
        
Comments
Post a Comment