NYOTA wa Real Madrid, Gareth Bale ameonyesha matumaini ya kupona haraka matatizo yake ya jeraha la enka baada ya kusema kuwa amekuwa akiimarika kila siku.
Hatua hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita nyota huyo kufanyiwa upasuaji wa enka, ambao aliupata wakati wa mchezo ambao Real Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sporting CP.
Hata hivyo, Bale ambaye aliripotiwa kuwa angeweza kukosekana uwanjani kwa muda wa miezi mine, jana alituma picha ya video kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter akiwashukuru mashabiki na kusema kuwa tatizo lake linakwenda vizuri.
"Uponaji wangu unakwenda vizuri. Tatizo langu la enka limekuwa likiimarika kila siku," aliandika kupitia ujumbe huo ulioambatana na picha hiyo ya video.
"Nawatakia kila la kheri wenzangu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Dortmund utakaopigwa leo ila nitauangalia nikiwa hapa nyumbani hala Madrid!" aliongeza.
Comments
Post a Comment