Depay ana mengi ya kufanya sasa hivi ili aendelee kufanya vizuri kwenye kiwango chake cha soka. Lakini kwa jinsi inavyoonekana amegoma na kuendelea na maisha yake binafsi ayapendayo ambayo ni kula bata hadi kuku aone wivu.
Kama anashindwa kumvuti Mourinho basi juhudi zange zingeweza kuzivutia hata club nyingine kubwa ambazo zingeweza kumpa dili zuri na kuendelea kucheza kwenye club kubwa zinashiriki mashindano kama UEFA Champions.
Lakini jamaa huyu amepigwa picha akiwa kwenye bar moja akitoa moshi kama treni. Hapo Depay alipigwa picha akivuta Shisha kitu ambacho hakitamvutia manager wake Jose Mourihno.
Shisha angeweza kuvuta hata akiwa nyumbani ambapo asingeweza kupigwa picha kama hii. Tusubiri mwezi wa kwanza kumuona akielekea Everton ambapo labda atapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza na kuonyesha uwezo ambao Mourihno ameshindwa kuuona.
Comments
Post a Comment