Carlos Tevez kutoka $2milion kwa mwaka hadi $20milion kwa mwaka.


Carlos Tevez kutoka $2milion kwa mwaka hadi $20milion kwa mwaka.

screen-shot-2016-12-29-at-3-07-14-pm
Ni mwendo wa pesa tu ndani ya China Super League ambapo Boca Junior wameshathibitisha kukubaliana na Shanghai Greeland Shenhua juu ya uhamisho wa mchezaji Carlos Tevez.

Zimelipwa kiasi cha dola za Marekani milioni 10 ili kumpata mchezaji Carlos Tevez mwenye miaka 32. Kwa upande wa Teves imeripotiwa kwamba atalipwa kiasi cha dola milioni 40 ndani ya miaka 2 huko China wakati alivyokua Argentina alikua analipwa milioni 2 kwa mwaka.

Mshahara wake umetajwa kwamba utakua kiasi cha pound 615,000 kwa wiki na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi duniani. Top 5 ya wachezaji wanaolipwa pesa nyingi duniani kwa sasa ni Teves, Oscar,CR7,Messi na Hulk. Watatu kati yao wote wapo kwenye ligi ya China.

screen-shot-2016-12-29-at-3-06-34-pm



Comments