Wiki iliyopita manager wa Manchester United alisema kwamba mchezaji wake Martial inabidi akaze buti ili aonyeshe thamani yake ndani ya kikosi. Jose alisema wachezaji ni marafiki lakini mwisho wa siku lazima wagombanie namba na mkali zaidi ndiye atakaye pata namba.
Baada ya Martial kufunga magoli mawili kwenye ushindi uliopita wiki hii Jose ameongea maneno mazuri kuhusu mchezaji huyo. "Martial anafanya kazi, anafanya kazi kwa bidii zaidi ya kusema kweli. Unapofunga mara mbili labda inaweza kusaidia kurudisha furaha na uaminifu kwamba umerudi kwenye level yako. Ukiwa mchezaji ambae unatakiwa kufunga unaweza kucheza vizuri lakini usipofunga furaha haikamiliki"
Kourihno anategemewa kuendelea kumtumia zaidi Martial baada ya kuweza kufunga mara mbili kwenye mchezo uliopita.
Comments
Post a Comment