THIBAUT COURTOIS AZITOLEA NJE ATLETICO, REAL MADRID... asema anajisikia furaha kubwa kuwepo Chelsea


THIBAUT COURTOIS AZITOLEA NJE ATLETICO, REAL MADRID... asema anajisikia furaha kubwa kuwepo Chelsea
MLINDA mlango Thibaut Courtois amezitolea nje timu mbili za La Liga ambazo zilikuwa katika orodha ya kumwania katika usajili wa dirisha la Januari mwakani.

Akikanusha mlinda mlango huyo alisema pamoja na kuakiwa na timu za Atletico na Real Madrid msimamo wake ni kutotaka kurejea kukipiga katika Ligi hiyo ya Hispania.
Kutokana na hilo Thibaut amesisitiza dhamira yake ya kutaka kubakia ndani ya kikosi cha matajiri wa Darajani Chelsea.

Courtois mwenye umri wa miaka 24 aliitumikia kwa mkopo Atltico Madrid na kuisaidia kushinda mataji ya Winning La Liga ikiwemo ubingwa wa Copa del Rey na ubingwa wa Ligi ya Ulaya.

Pia aliisaidia Atletico kufikia fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya mnamo mwaka 2014.

Akinukuliwa mlinda mlango huyo amesema kwa sasa anajivunia hatua ya kuaminika kama nambari moja ndani ya Chelsea hatua inayompa faraja kubwa.

"Ninachoweza kusema ni kwamba sijazungumza na timu yoyote kati ya Atletico ama Real Madrid hivyo taarifa zote za uvumi ni uzushi mkubwa."


"Nina jisikia furaha kuwepo hapa Chelsea nina heshima kubwa hapa hivyo sitarajii kuondoka kwa sasa."


Comments