NI wazi mashabiki wa Chelsea wamesahau wakati mshambuliaji wao kinara wa mabao Ligi Kuu England kwa sasa, Diego Costa alipoonyesha dhamira kurudi Atletico Madrid.
Lakini kitendo cha Costa kupiga picha akiwa na kocha wa Atletico, Diego Simeone wakifurahia chakula cha jioni, kimewashitua.
Costa kwa sasa yuko Hispania kwa ajili ya kuchezea timu ya taifa mechi ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Macedonia.
Kuwepo kwake nyumbani Hispania kulimpa fursa ya kukutana na marafiki na kocha wake wa zamani.
Costa alituma picha kwenye mtandao wa kijamii akiwa na kocha wake wa zamani na kuandika: "Furaha kubwa kuungana tena."
Zaidi ya watu 35,000 waliipenda picha hiyo, huku wengine 500 wakiandika ujumbe.
Baadhi ya watu waliotuma ujumbe kuhusiana na picha hiyo waliwaponda mashabiki wa Chelsea ambao miezi mitatu iliyopita walisikika kauli ya mchezaji huyo kutaka kuondoka.
Comments
Post a Comment