RONALDO AZIDI KUIPAISHA REAL MADRID ...apiga mbili Sporting Gijon ikifa 2-1



RONALDO AZIDI KUIPAISHA REAL MADRID ...apiga mbili Sporting Gijon ikifa 2-1

Real Madrid imeifunga Sporting Gijon 2-1 kwenye mechi ya La Liga iliyochezwa  Santiago Bernabeu huku Cristiano Ronaldo akifunga yote mawili na kuwa kinara wa ufungaji.

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye fomu ya kutisha, alifunga la kwanza dakika ya 5 kwa njia ya penalti na la pili akatupia dakika ya 18.

Bao pekee la Sporting Gijon likafungwa na kiungo Carlos Carmona kunako dakika ya 35.


REAL MADRID (4-4-2): Keylor 6; Danilo 6, Pepe 6, Ramos 6 (Marcelo, 72, 6), Nacho 7; Lucas 7, Kovacic 6 (Isco, 81), Modric 6, Rodriguez 6 (Asensio, 72 6); Benzema 6, Ronaldo 8

SPORTING GIJON (5-4-1): Marino 6; Douglas 6, Lillo 6, Mere 7, Amorebieta 6, Lopez 6; Alvarez 6, Rachid 6 (Cases, 81), Carmona 7 (Rodriguez, 76, 6), Moi Gomez 7 (Viguera, 76); Cop 6




Comments