Messi awalipa walinzi wa Argentina kwasababu chama hakijawalipa.


Messi awalipa walinzi wa Argentina kwasababu chama hakijawalipa.

screen-shot-2016-11-19-at-4-53-17-pm
Chama cha soka cha Argentina hakijawalipa walinzi wa timu kwa muda wa miezi sita lakini walinzi hao wakuacha kufanya kazi. Kazi yao ilikua ni kulinda kikosi hicho kiwe salama kokote wanapoenda.

Walinzi hao wakiwa kazini walikubaliana kwamba wamfikishie tatizo lao captain wa timu hiyo Lionel Messi ili aweze kuwasaidia mbele ya chama cha soka cha Argentina. Ripota mmoja wa huko Argentina alisema kwamba walinzi hao walimfata captain na kumueleza tatizo lao.

Baada ya Messi kuwasikiliza moja kwa moja akampigia simu baba yake na kumwambia ashugulikie tatizo hilo kwa kuwalipa walinzi hao ambao walikua wanafanya kazi nzuri ya kukiweka kikosi salama muda wote.

Baada ya habari hizi kutoka watu wote walimsifia Messi kwa kuonyesha hali ya kuwa kiongozi bora kivitendo.Fifa wamekua wakiangalia chama cha soka cha Argentina kwa muda mrefu baada ya skendo na uchunguzi wa kutumia pesa vibaya.



Comments