Inaonekana kama Mourinho alikuwa kituko kwenye uwanja wa Old Trafford kwasababu vitendo vyake vilimfanya mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey ashindwe kujizuia kucheka mbele ya sura ya Mourinho.
Jose Mourinho alikasirika sana baada ya timu yake kunyimwa mkwaju wa penati dhidi ya Arsenal.
Mara zote amekuwa akiwalaumu waamuzi pale anapoona wanatoa maamuzi tofauti na anavyofikiria akiamini hawaitendei haki timu yake.
Inatajwa kwamba, United ni timu ambayo imefaidika sana kwa mikwaju ya penati ndani ya Premier League, hivyo inaonesha Mourinho anapenda utamaduni huo uendelee.
Aliondolewa kwenye benchi wakati timu yake ikikabiliana na Bournemouthna huenda angetolewa pia kwenye mchezo wa leo kutokana na kitendo chake cha kulalama kwa mwamuzi baada ya Antonio Valencia kuangushwa kwenye eneo la hatari na mwamuzi hakuamuru kupigwa kwa mkwaju wa penati.
Comments
Post a Comment