GWIJI wa zamani wa Arsenal Martin Keown amesema kutokuwepo kwa Zlatan Ibrahimovic kwenye kikosi cha Manchester United katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Arsenal si jambo linalostahili kushangiliwa na vijana wa Arsene Wenger.
Ibrahimovic atakosekana kufuatia kuwa na kadi tano za njano na nafasi yake inatarajiwa kuzibwa ipasavyo na kinda Marcus Rashford.
Keown ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka, amesema Rashford ni hatari zaidi kwa namna alivyo na uchu na nyendo za hatari anapolikabili lango la adui.
Comments
Post a Comment