MANCHESTER UNITED YAFUFUKA KWA SWANSEA ...Zlatan Ibrahimovic atupia mbili, Pobga wee wacha tu, Rooney usipime
MANCHESTER UNITED imecharuka na kuvuna ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Swansea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Paul Pogba alifunga bao tamu dakika ya 15 katika 'muvu' ambayo aliianzisha mwenyewe kabla ya kuachia mkwaju wa mbali uliokwenda moja kwa moja wavuni.
Ilikuwa siku njema kwa Zlatan Ibrahimovic ambaye alifunga mara mbili dakika ya 21 na 33 na kumaliza ukame wa muda mrefu wa kutoka uwanjani bila goli katika mechi za Premier League.
Bao pekee la Swansea lilifungwa na Mike van der Hoorn dakika ya 69 huku kocha wa Manchester United akiutazamia mchezo huo jukwaani kufutia kufungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi moja.
Nahodha Wayne Rooney amerejeshwa kwenye kikosi cha kwanza na kuwa nyota wa mchezo huku msaidizi wake Michael Carrick naye akianzishwa na kutakata vilivyo.
SWANSEA (4-4-2): Fabianski 5.5; Rangel 5, Van der Hoorn 6, Mawson 6, Kingsley 5.5; Routledge 4 (Barrow 46mins, 5.5), Britton 5 (Fer 70, 5), Ki 5, Sigurdsson 5.5; Borja Baston 5, Llorente 4 (Montero 46, 5)
MANCHESTER UNITED (4-3-3): De Gea 6; Young 6, Jones 6.5, Rojo 6.5, Darmian 6; Carrick 7, Fellaini 6.5, Pogba 6.5 (Fosu-Mensah 90+4); Mata 6.5 (Lingard 82), Rooney 8 (Schneiderlin 89), Ibrahimovic 7.5
Zlatan Ibrahimovic akishangilia kwa staili ya Kung Fu
Ibrahimovic amefanikiwa kuondoa ukame wake wa magoli
Paul Pogba akiifungia United bao la kwanza
Pogba akibusu gloves kufurahia goli lake dhidi ya Swansea
Comments
Post a Comment