HATMA ya Luke Shaw na Chris Smalling ndani ya Manchester United iko mashakani baada ya kocha Jose Mourinho kusema baadhi ya wachezaji wake hawana uwezo wa kujitoa muhanga na kucheza wakiwa na maumivu.
Mabeki hao wa England walikosekana katika mchezo wa Premier League wa ushindi wa 3-1 dhidi Swansea Jumapili iliyopita baada ya kumwambia Mourinho kuwa hawawezi kucheza.
Mourinho naye akaanzisha mashambulizi ya kiaina wakati akifanya mageuzi kwenye safu yake ya ulinzi kwa kusema: "Tuna wachezaji wenye matatizo."
Kocha huyo akawasilisha ujumbe huo hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mbele ya wachezaji na kutoa taswira kuwa wawili hao hawana nafasi tena Manchester United.
"Luke Shaw aliniambia kuwa hayuko katika hali nzuri kuweza kucheza dhidi ya Swansea, hivyo tulipaswa kujenga upya safu yetu ya ulinzi. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mchezaji ambaye yupo tayari kucheza kwa gharama yoyote na mchezaji anayehofia kuingia uwanjani kwasababu tu ana maumivu madogo," alisema Mourinho.
Kocha huyo alimpongeza Smalling mwenye umri wa miaka 26 kwa kucheza mchezo wa kipigo cha 4-0 dhidi ya Chelsea Oktoba 23 huku akiwa amechomwa sindano za kuzuia maumivu lakini katika mechi ya Swansea Mourinho akasema: "Smalling hajisikii kama anaweza kucheza kwa asilimia 100 kwa maumivu aliyonayo."
Kocha Manchester United Jose Mourinho akiwa jukwaani kwenye mchezo dhidi ya Swansea
Luke Shaw (pichani) na Chris Smalling wamelikoroga kwa Mourinho
Smalling (kulia) hakucheza dhidi ya Swansea
Comments
Post a Comment