MWEZI Oktoba              mwaka jana Liverpool ilimtangaza rasmi kocha Jurgen Klopp              kurithi mikoba ya Brendan Rodgers. Klopp alikuwa ametoka              mapumzikoni baada ya kuachana na klabu ya Borussia Dortmund              ambayo aliipa mataji yote muhimu ndani ya Ujerumani.
        Mbali na mataji              ya ndani, pia kwenye michuano ya Ulaya Dortmund chini ya              Klopp ikafika fainali ambayo walipoteza dhidi ya wapinzani              wao, Fc Bayern Munich kwenye uwanja wa Wembley.
        Ni takriban mwaka              mmoja umepita tangu Kloipp aingie kandarasi ya miaka mitatu              kuwafundisha majogoo wa Anfield.
        Miezi minne tangu              alipojiunga na Liverpool, Klopp alifanikiwa ucheza fainali              ya Kombe la Ligi bahati mbaya akapoteza dhidi ya City kwa              penati 3-1.
        Mwezi Mei mwaka              huu wakapoteza tena fainali nyingine dhidi ya Sevilla kwenye              michuano ya Europa.
        Kabla ya hapo              Liverpool ilikuwa haijafanikiwa kutinga hatua yoyote ya              fainali michuano ya Ulaya tangu mwaka 2007.
        Wikiendi hii              Liverpool imekaa kwenye kilele cha msimamo wa Ligi kwa mara              ya kwanza chini ya Jurgen Klopp.
        Kwenye Ligi yenye              Pepo Guardiola, Antonio Conte, Maurcio Pochettino, Arsene              Wenger na Jose Mourinho sio jambo rahisi.
        Liverpool ina              wastani mzuri wa mabao hadi sasa, hakuna timu ambayo inaweza              kutikisa nyavu za wapinzani mara 30 ukiondoa Liverpool. Timu              inacheza soka la uhakika lenye ladha zote, mabao na              burudani.
        Pointi 26n              zimetisha kumweka Klopp kwenye nafasi ya kwanza tangu              alipojunga na Liverpool tangu takriban mwaka mmoja uliopita.
        Tofauti na msimu              uliopita ambao alikuta tayari timu imeshasajiliwa na              Rodgers, msimu huu Klopp amefanya usajili mwenyewe na pia              ametengeneza aina ya timu anayoitaka mwenyewe. Klopp ni              miongoni mwa makocha wanaoonekana kufanikiwa kimfumo msimu              huu wa Ligi Kuu nchini Uingereza.
        Ana nafasi kubwa              ya kuipeleka Liverpool kwenye mafanikio mapya ya kunyakua              taji la Ligi Kuu nchini humo ambalo wamelikosa kwa miaka              takriban 26.
        Pep Guardiola              alionekana aipanda na kushuka akiwa na kikosi chake cha Man              City. Tayari hadi sasa amepoteza pointi sita baada ya kutoka              sare tatu kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Etihad Stadium.
        Jose Mourinho              bado anajikongoja na kikosi chake cha Manchester United kama              ilivyo kwa Mauricio Pochetino ambaye anapoteza pointi nyingi              kwa kutoka sare kwenye michezo ya EPL.
        Wapinzani ambao              wanaweza kuzima ndoto za Klopp ni Antonio Conte ambaye              amefanikiwa kuingiza mfumo wake wa Kitaliano maarufu kama              "Catenaccio" pale Chelsea. 
        Mwingine ni              Arsene Wenger lakini kwa bahati mbaya huwa anaanza Ligi              vizuri na kumaliza vibaya.
        Klopp anaweza              kuifikisha Liverpool kwenye mafanikio ya kina Bill Shankys.              Bahati nzuri Liverpool kwa sasa sio timu ambayo ina presha              kubwa kuifundisha kama ilivyo kwa Manchester United na              Chelsea.
        Huyu ni miongoni              mwa makocha ambao wanaweza kukupa mafanikio kwenye timu yako              tena kwa kutumia koiasi kidogo tu cha fedha. Baada ya mwaka              mmoja tangu ajiunge na majogoo ameshika nafasi ya kwanza              kwenye Ligi. Je, ikifika mwezi Mei mwakani atakuwepo tena              kwenye nafasi hiyo? Tusubiri tuone.
        
Comments
Post a Comment