VINARA wa Ligi ya              Serie A, Inter Milan wameanza kuwafukuzia nyota wanne wa              Manchester United, Chris Smalling, Memphis Depay, Daley              Blind na Matteo Darmian, ili kuona kama itaweza kuwanasa              wakati dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mapema              Januari.
        Kwa mujibu wa              gazeti la Corriere dello Sport, timu ya Inter Milan iko              karibu na kocha Jose Mourinho baada ya kupata mafanikio na              klabu hiyo ya San Siro kuanzia mwaka 2008 – 2010 na mbali na              hilo pia Mourinho anasemekana kuwa karibu na makamu wa rais              Javier Zanett, mkurugenzi wa michezo Piero Ard na kocha mpya              Stefano Pioli.
        
Comments
Post a Comment