Kila mtu anafika kwenye level ya juu ya mafanikio kwa juhudi          zake na pia kwa msaada wa watu wake wa karibu. Cristiano Ronaldo          leo hii anaonekana kuwa ni mchezaji wa kiwangi cha juu lakini          hawa hapa ni watu nane ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa          kufika hapa alipofika.
Laszlo Boloni
          Hutu ndiye kocha wa Ronaldo aliyempa nafasi ya kwanza kuwa          mchezaji professional kwenye club ya Sporting Lisbon. CR7          alicheza hapa na kukua kabla ya hajahamia United ambapo umaarufu          wake ndio uliongezeka.
Sir Alex Ferguson
          Scotsman alimchukua Ronaldo mwaka 2003 na akakaa nae kwa muda          miaka 6 akiingia kwenye mafanikio ya kushinda mataji makubwa ya          soka. Ronaldo siku zote anamchukulia Sir Alex kama baba yake          kwenye ulimwengu wa soka.
Carlos Queiroz
          Kocha msaidizi wa Manchester united alimfanya Ronaldo kuwa          comfortable wakati yupo Manchester hasa kwenye miaka ya          mwanzoni. Licha ya Ronaldo kuwa karibu sana na Sir Alex lakini          alikua na connection ya karibu na Carlos kutokana na kuwa          wanatoka wote Portugal na wanaongea lugha moja ya nyumbani.
Jorge Mendes
          Wakala wa Ronaldo amefanya kazi kubwa ya kumtafutia kazi nzuri          zenye malipo makubwa na kumjengea Ronaldo mafanikio makubwa          kibiashara. Ronaldo analipwa vizuri na kampuni mbalimbali          kutokana na kazi kubwa ya Jorge Mendes.
Rio Ferdinand
          Richa ya Roy Keane kuwa captain kwa wakati Ronaldo anaingia          United, Ferdinand ndio alikua kama kaka mkubwa kwa CR7. Alikua          karibu na Ronaldo wakati wote wakiwa kwenye dressing room.
Luiz Felipe Scolari
          Huyu ndiye kocha ambaye alifanya ndoto za Ronaldo kuwa za kweli          baada ya kumpa majukumu kwenye timu ya taifa ya Portugal kwa          mara ya kwanza.
Comments
Post a Comment