Giroud amekuwa mchezaji wa kwanza wa Arsenal kufunga bao dhidi ya timu inayofundishwa na Mourinho ndani ya Premier League tangu May 2007 ambapo Gilberto Silva alifunga kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Emirates.
Rekodi ya Mourinho dhidi ya Wenger na Arsenal ni ya kutukuka, hajawahi kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal wala Arsene Wenger na wakati Mourinho yupo Chelsea, ilonekana angepata ushindi kila alipokutana na The Gunners.
Kuna wakati Didier Drogba alikuwa akihofiwa na mabeki wa Arsenal ambao walijua angefunga hata kabla hawajaingia uwanjani.
Lakini angalau kwenye mchezo wa leo wameweza kufunga goli dhidi ya timu ya Jose Mourinho.
Rekodi
- Goli lililofungwa na Giroud kwenye sare ya 1-1 lilikuwa ni goli la kwanza kwa mchezaji wa Arsenal kufunga kwenye ligi dhidi ya timu inayonolewa na Mourinho tangu mwaka 2007.
- Ni msimu wa 2004-05 pekee ndiyo Manchester United ilikuwa na pointi chache (18) baada ya mechi 12 za Premier League lakini kwa sasa wanapointi 19 hadi sasa.
- Ni Wayne Rooney pekee ndiye aliyefunga magoli mengi kwenye Premier League (29) tangu Juan Mata alipocheza mechi yake ya kwanza baada ya kujiunga na United January 2014 huku Mata mwenye akiwa ameshafunga mara 24.
- Manchester United wametoka sare ya tatu mfululizo kwenye uwanja wa Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu April 1999.
- Arsenal wameshindwa kupiga shuti lililolenga lango ndani ya kipindi cha kwanza ndani ya Premier League kwa mara ya kwanza tangu April mwaka huu walipocheza dhidi ya Norwich City.
Comments
Post a Comment