Dwayne Wade arejea nyumbani na kumwadhibu baba yake.


Dwayne Wade arejea nyumbani na kumwadhibu baba yake.

i Dwyane Wade ameitumikia klabu ya  Miami Heat kwa miaka 13, kaifanyia mengi, kaitumikia kwa moyo wote mpaka akafikia hatua ya kuitwa "Mr. Miami". Huyu walimimwita ushindi wao wa kila siku.

Alfajiri ya leo alikuwepo tena South Beach Miami lakini kipindi hiki hakuwepo ili kuwapa furaha mashabiki wa Miami. Kipindi hiki alikuja na klabu yake mpya ya nyumbani kwao, Chicago Bulls.

Wade aliiongoza Chicago Bulls kuichapa Miami 98-95 na kuhakikisha kuwa sehemu aliyoiita nyumbani kwa kipindi cha miaka 13 anapata ushindi dhidi yake kwa mara ya kwanza.

"Naweza kuwaza tu na kufikiri hali aliyokuwa anaipitia siku ya leo," kocha wa Bulls Fred Hoiberg alisema. "Kulikuwa na hisia kali sana kurejea tena eneo hili."

Jimmy Butler alifunga pointi 20 na Rajon Rondo alimaliza mchezo akiwa na pointi 16 na assist 6 na rebound 12 kwa upande wa Bulls. Robin Lopez aliongeza pointi 16 huku Wade akifunga pointi 13.

Winslow alifunga pointi 15 na Tyler Johnson akaongeza 14 kwa upande wa Miami.

HIGHLIGHTS

 



Comments