DANIEL STURRIDGE MBIONI KUIMWAGA LIVERPOOL BAADA YA KUCHOSHWA NA BENCHI


DANIEL STURRIDGE MBIONI KUIMWAGA LIVERPOOL BAADA YA KUCHOSHWA NA BENCHI
STAA Daniel Sturridge anasemekana kuwa yuko tayari kuitema klabu yake ya Liverpool kwa kile kinachodaiwa ni kukerwa na kuwekwa benchi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, straika huyo wa timu ya taifa ya England hana raha kwenye klabu hiyo ya Anfield na huenda akaondoka kwenye klabu hiyo ya Merseyside wakati wa usajili wa majira ya baridi yajayo.


Kutokana na hali hiyo, klabu mbalimbali zimeshaanza kupiga jaramba baada ya kubaini kuwa Sturridge hayuko katika mipango ya kocha wake Jurgen Klopp.


Comments