Best Quote za uadui kati ya Wenger na Mourinho.


Best Quote za uadui kati ya Wenger na Mourinho.

screen-shot-2016-11-19-at-4-22-21-pm Jose Mourinho na Wenger leo wanaziongoza timu zao kucheza mechi nyingine kwenye ligi ya England. Sasa kutokana na historia ya ugomvi wao wa maneno hizi hapa ni Quote ambazo zimetokana na maneno kati yao.
2015:
Jose Mourihno : "Ninaogopa kufeli, Yeye (Wenger) amebobea kwenye kufeli mimi hapana. Sasa kama swala kufeli ni kweli mimi naogopa kufeli kwasababu sifeli mara zote na wala kufeli sio kitu changu. Lakini yeye(Wenger) ni mtaalamu wa kufeli kwasababu miaka nane hajapata chochote cha kujivunia"

2005:
Arsene Wenger: "Yeye(Mourihno) yupo nje ya utaratibu na kiukweli hana adabu. Ukiwapa mafanikio watu wasiokuwa na akili akili zinawatoka zaidi ya kuongezeka"
2010: Wenger akizungumzia jinsi Madrid ilivyocheza kwenye UCL.
Arsene Wenger: "Ukiangalia kwenye Tv ni njia nzuri ya kuona kwamba hawatakiwi kufanya vile tena. Ni kitu kibaya wamefanya kutoka kwenye club kubwa"
2010: Morinho akamjibu
Jose Mourihno: "Badala ya Wenger kuzungumzia Real Madrid inabidi azungumzie Arsenal. Kupoteza kwake wa 2-0 ni fundisho kwake kwamba historia ya watoto wadogo kwenye kikosi chake imesha sasa hivi. Sagna, Walcott, Fabregas, Nasri, Van Parsie sio watoto tena ni watu wazima".
2015: Mourinho amdhihaki Wenger
"Kuna makocha wengine kwa mara ya mwisho wameshinda taji ni miaka 10, mimi nimeshinda mwaka mmoja uliopita. Kama kuna kitu cha ku-prove tayari ninacho. Fikiria wengine walivyo wakati sisi kwetu kumaliza nafasi ya nne sio lengo letu."



Comments