ARSENAL imepunguzwa kasi na Tottenham baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo Ligi Kuu ya England.
Harry Kane ndiye aliyefuta matumaini ya Arsenal kukaa kileleni mwa Ligi Kuu kwa kuifungia Tottenham bao la kusawaisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 51, hiyo ikiwa ni mara yake ya nne kuitungua Arsenal katika mechi tano zilizopita.
Kevin Wimmer aliizawadia Arsenal bao la kuongoza baada ya kujifunga dakika ya 42 na kuwafanya vijana wa Wenger waende mapumziko wakiwa mbele.
ARSENAL XI (4-2-3-1): Cech 6.5; Bellerin 7, Mustafi 5, Koscielny 6, Monreal 6.5; Coquelin 6.5 (Ramsey 65mins, 5), Xhaka 7; Walcott 6 (Oxlade-Chamberlain 71, 5), Ozil 7, Iwobi 5.5 (Giroud 70, 5); Sanchez 5.5
TOTTENHAM XI (3-4-1-2): Lloris 7; Dier 6.5, Wimmer 5.5, Vertonghen 7; Walker 5.5 (Trippier 80), Wanyama 7, Dembele 7.5, Rose 6.5; Eriksen 6.5; Son 5.5 (Winks 89), Kane 6.5 (Janssen 73, 5)
Harry Kane wa Tottenham akishangilia bao kusawazisha
Kane akiusukumiza mpira wavuni kwa penalti
Kevin Wimmer akijifunga na kuipa Arsenal bao la kuongoza
Comments
Post a Comment