ZLATAN IBRAHIMOVIC AMTANIA WAKALA WA POGBA "NITAKUVUNJA MGUU UKIMRUHUSU MCHEZAJI WAKO KUONDOKA MAN UNITED"
MSHAMBULIAJi mpya wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amemfanyia mzaha wakala Mino Raiola wa kiungo Paul Pogba kwamba atamvunja mguu iwapo atamruhusu mchezaji huyo kujiunga na klabu nyingine.
Ibrahimovic amesema Pogba ni mchezaji muhimu kwa Manchester United na ataanza kuonyesha vitu vyake hivi karibuni. Pogba hivi karibuni aliifungia Manchestrer United bao moja kati ya manne ilipowapiga mweleka wa mabao 4-1 Leicester City.
Comments
Post a Comment