WACHEZAJI WABAGUZI KUFANYA MAZOEZI NA WANAWAKE



WACHEZAJI WABAGUZI KUFANYA MAZOEZI NA WANAWAKE
WACHEZAJI wawili wa timu ya soka ya Sparta Prague wameambiwa kufanya mazoezi na timu ya wanawake baada ya kutoa matamshi ya kiubaguzi dhidi ya maafisa wanawake wanaosimamia mechi.

Kipa Tomas Koubek mwenye umri wa miaka 24, alisema kuwa: "Wanawake wanafaa kuwa jikoni baada ya naibu refa Lucie Ratajova kushindwa kuinua bendera kwa mchezaji ambaye alikuwa ameotea wakati wa mechi ya siku ya Jumapili ambapo walitoka sare ya 3-3 na Brno.

Kiungo wa kati, Lucas Vacha mwenye umri wa miaka 27 alichapisha picha katika mtandao wake wa Twitter ikiwa na matamshi: "Waelekee jikoni."

Ofisa mkuu wa klabu ya Sparta, Adam Kotalik aliyataja matamshi hayo kama yasiyokubalika.

akizungumza baada ya mechi ya Jumapili, raia huyo wa Jamhuri ya Czech aliongezea: "Wanawake hawafai kusimamia mechi za wanaume."


Baadae alichapisha picha ya mkwe na mwanawe wa kike katika mtandao wa facebook na kusema "Ningependa kuomba msamaha kwa wanawake wote."


Comments