Utafiti: Messi nafasi ya 4, Ronaldo nafasi ya 23 list ya wachezaji bora wa muda wote La Liga


Utafiti: Messi nafasi ya 4, Ronaldo nafasi ya 23 list ya wachezaji bora wa muda wote La Liga

ronaldomessi-la-liga

Kuna list imetoka inayowahusu wakali wawili wa La Liga Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambayo imeibua mijadala mikubwa.

Umefanyika utafiti unaohusisha historia na takwimu za soka la Hispania ambao umeweka hadharani orodha ya wachezaji bora kuwahi kutokea katika miaka 85 ya historia ya La Liga.

Utafiti huo kuhusu La Liga umefanywa na Antonio Ortega, ambaye amefanya uchambuzi wa wachezaji 9,000 waliowahi kucheza kwa mafanikio nchini Hispania kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1920.

Utafiti huo ulizingatia ufungaji, assists, blocks, fouls pamoja na idadi ya magoli ya kufunga.

Kwa mujibu wa vigezo vilivyotumika katika utafiti huo, pointi 24 zilitolewa kwa kila mchezaji kulingana na dakika alizocheza kwa msimu, pointi moja kwa kila goli la kufunga, 0.6 kwa goli la penati, lakini pointi zilikuwa zinakatwa pia. Kwa mfano, goli la kujifunga lilikatwa pointi 0.4 huku kila mchezaji alipooneshwa kadi nyekundu alikatwa pointi 1.5.

Utafiti umebaini kuwa, mchezaji bora wa muda wote ni mkongwe wa Real Madrid Raul Gonzalez.

Mkongwe wa Barcelona César Rodriguez anakamata nafasi ya pili huku Telmo Zarra wa Athletic Bilbao akichukua nafasi ya tatu.

Lionel Messi ameshika nafasi ya nne katika orodha hiyo.

Mchezaji wa zamani wa Sporting Gijon na Barcelona Enrique Castro 'Quini' amekaa kwenye nafasi ya tano

Juan Arza, Alfredo di Stéfano, Francisco Gento, Carlos Alonso 'Santillana' na Guillermo Gorostiza wanakamilisha top 10.

Utafiti huo umezingatia dakika ambazo mchezaji amecheza ndani ya La Liga na kumwacha Ronaldo katika nafasi ya 23.

Star huyo wa Ureno amewapiku wakali wengine waliocheza kwa ligi ya Hispania ikiwajumuisha David Villa (32), Xavi Hernandez (49), Iker Casillas (62) pamoja na Aritz Aduriz (109).

Top 5 ya wachezaji bora kuwahi kutokea La Liga (kwa muji wa utafiti huu)

Raul Gonzalez – 528 points

César Rodriguez – 524 points

Telmo Zarra – 493 points

Leo Messi – 490 points

Enrique Castro 'Quini' – 488 points



Comments