Baada ya Uganda kupangwa Kundi D sambamba na timu za Misri, Ghana, pamoja na Mali kwenye micuano ya AFCON 2017, kocha wa Uganda Cranes Micho Sredojević ametoa wito kwa serikali kuhakikisha timu inapata support ya kutosha kwa ajili ya maandalizi ya mapema.
Licha ya timu yake kupangwa kwenye Kundi gumu, Micho hana budi bali ni kupambana na changamoto iliopo mbele yake.
"Hakuna namna ya kukwepa, unaweza ukasema pengine ndiyo mwisho wetu, ni sawa na Kundi tulilopo kwenye Kombe la Dunia lakini safari hii ni fainali za AFCON dhidi ya Ghana na Misri. Ni kundi gumu lenye ushindani," alisema Micho mara baada ya draw ya upangaji makundi kukamilika.
Ghana walipoteza kwenye mchezo wa fainali katika michuano iliyopita ya FCON iliyofanyika Equatorial Guinea 2015 dhidi ya Ivory Coast. Misri ni nchi yenye uchu ikiwa imeyakosa mashindano hayo kwa miaka misimu mitatu iliyopita, lakini wakiwa ni mabingwa mara tatu mfululizo waliopta, Mali ndani ya fainali tatu za AFCON wameshika nafasi ya tatu mara mbili, ni kundi gumu.
Ghana na Uganda zilitoka suluhu kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kundi E kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na wanatarajia kucheza mara mbili dhidi ya Misri baada ya michuano ya AFCON kumalizika.
"Ukiangalia kila kitu, utaona tunatakiwa kuanza maandalizi sasa kwa upendo na support kutoka waganda wote, wachezaji na wote wenye wajibu wa kuiandaa timu yetu kuwa timu yenye ushindani, hapa nafikiria maandalizi pamoja na mechi za kirafiki ambapo tutakuwa makini na kila taarifa. Naamini katika soka hakuna kinachoshindikana bali kila kitu kinawezekana."
"Ninaiamini timu na wachezaji tulionao, naamini katika kile tunachokifanya, ninaamini serikali ya Uganda itatusaidia kuhakikisha tunaliwakisha taifa katika njia bora."
"Hatua tuliyofikia ni nusu ya safari, ili safari yetu ikamilike tunahitaji kuanza maandalizi sasa, tunastahili kuwa hapa lakini tunahitaji kuonesha hilo kwa vitendo tukiwa uwanjani na si kwa kuongea."
Uganda wataanza kampeni yao kwa mchezo wao wa ufunguzi January 17 dhidi ya The Black Stars, kisha watashuka tena uwanjani kukabiliana na mapharao wa Msri January 21 kabla ya kuhitimisha hatua ya makundi dhidi ya Mali January 25.
Makundi
GROUP A: Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea Bissau
GROUP B: Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe
GROUP C: Cote D'Ivoire, DR Congo, Morocco, Togo
GROUP D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda
Comments
Post a Comment