TOTTENHAM HOTSPURS inatajwa kuwa tayari kuvunja rekodi yao ya manunuzi kwa kutoa kitita cha paundi milioni 40 ili kumsajili Isco kutoka Real Madrid Januari mwakani.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akihangaika kupata nafasi katika kikosi cha Zinedine Zidane, akianza katika mechi mbili pekee msimu huu na alikuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Spurs kipindi cha kiangazi.
Isco aliyenunuliwa na Madrid kutoka Malaga miaka mitatu iliyopita tayari ameeleza nia yake ya kuondoka kama atakosa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Comments
Post a Comment